Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandara ya Tanzania (Tanzania Port Authority) Eng. Kakoko na ujumbe wake walifanya ziara ya siku tatu visiwani komoro kuanzia tarehe 25-28 Juni 2018; dhumuni ya ziara hiyo ilikuwa kuja kutambulisha shughuli zinazofanywa na mamlaka ya bandari Tanzania, kutanua soko ya TPA na kutangaza bandari za Tanzania pamoja na kusikiliz changamoto zinazowakabili wafanyabiashara kutoka komoro pindi wanaposafirisha mizigo yao kutoka bandari ya Mtwara na DSM kuja Komoro.