Kwa masikitiko makubwa, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro unasikitika kuwajulisha msiba wa Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  (1925 - 2024), uliotokea tarehe 29 Februari 2024. 

Kufuati kifo hicho, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza siku Saba za Maombolezo kuanzia Ijumaa tarehe 1 Machi 2024 hadi Alhamis tarehe 7 Machi 2024. Maziko ya Marehemu Ali Hassan Mwinyi yatafanyika tarehe 2 Machi 2024 katika kijiji cha Mangapwani - Zanzibar. 

Kwa upande wake, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro utafungua kitabu cha Maombolezo kuanzia tarehe 1 Machi 2024 hadi tarehe 7 Machi 2024 kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana, ili kutoa fursa kwa wananchi na Viongozi kutoa salamu za pole. 

INNAA LILAAHI WAINNAA ILAYHI RAAJIUUN