Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro utaandaa Maonesho ya Biashara ya Bidhaa na Huduma za Tanzania nchini Comoro kuanzia tarehe 12 - 19 Desemba 2022. Maonesho hayo yatafanyika katika eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalopatika EGT, Moroni na kutoa fursa kwa Taasisi za umma na binafsi, Wafanyabiashara na Wajasiriamali kutoka nchi mbili hizi kutangaza bidhaa na huduma zao.
Ratiba ya Ufunguzi wa Maonesho hayo itafanyika tarehe 14 Desemba 2022 ambapo Mgeni rasmi ni Mheshimiwa Kanali Ahmed Abbas Ahmed, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Inatarajiwa kwamba wajasiriamali mbali mbali kutoka nchi mbili hizi watatumia fursa hiyo kujitangaza.