Kwa Masikitiko tumepokea na kusambaza kifo cha Mheshimiwa Edward Lowasa, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1953 - 2024) kilichotokea Jijini Dar es Salaam - Tanzania. Taarifa za mazishi zitatolewa hivi punde. 

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kumkumbuka kwa uongozi wake, hekima na busara zake katika kuwatumikia wananchi wote wa Tanzania. Aliweka mbele masilahi ya Taifa na kushinda tamaa binafsi au masilahi ya wachache. 

Mungu aipumzishe Roho ya Marehemu mahala pema Aamin.