Mheshimiwa Mahamoud Fakridine, Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Comoro amefanya ziara ya kikazi nchini Tanzania tarehe 23 - 25 Machi, 2023. Wakati wa ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri Mahamoud Fakridine aliambatana na Mheshimiwa Mohamed Ali Youssoufa, Waziri wa Ulinzi nchini Comoro pamoja na Maafisa Waandamizi. Akiwa nchini Tanzania, Mheshimiwa Waziri alionana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Hamad M. Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo Viongozi hao walifikia maazimio ya kuendeleza ushirikiano.