Ujumbe kutoka Hospitali ya Aga Khan ya nchini Tanzania ukiongozwa na Dkt. Fatma Bakshi, Mtaalamu wa Neva (Neurologist) umekutana na Mheshimiwa Pereira A. Silima, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro walipofika Ubalozini kwa lengo la kujitambulisha. Ujumbe huo umejulisha kuwa unaendelea na ziara ya siku tatu nchini Comoro kwa lengo la kuangalia fursa ya kuimarisha ushirikiano na hospitali za umma nchini humo.  Imefahamika kwamba Hospitali ya Aga Khan nchini Tanzania imekuwa kituo muhimu kwa kuwapatia huduma ya afya raia mbali mbali wa Comoro wanaoifika nchini Tanzania kupata huduma hiyo muhimu.