Ujumbe kutoka hospitali ya Agakhan Tanzania ulifanya ziara ya siku tatu Visiwani Comoro kwa ajili ya kuangalia fursa ya kufangua hospitali za Agakhan Visiwani hapa.Ujumbe huo uliwasili Comoro tarehe 21 Februari, 2019 na uliangozwa na Bw. Olayce Steven Lotha.

Wakati wakiwa ziarani Visiwani hapa ujumbe huo ulipata fursa pia ya kuonana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania Visiwani Comoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Ubalozi hapa Moroni na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara ya Afya ya Comoro.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Balozi alichukua fursa hiyo kupongeza Uongozi wa hospitali ya Agakhan kwa kuwa na dhamira ya kufngua hospitali yao hapa na kueleza kwamba hii ita punguzia gharama za matibabu kwa Wakomoro ambao wanasafiri nchi za mbali ikiwemo Tanzania kwa ajili ya kupata huduma za matibabu.

Hata hivyo, Mhe. Balozi aliuomba Uongozi wa Agakhan kupunguza gharama za matibabu kwani sehemu kubwa ya jamii ya Wakomoro ni watu wanyonge na maskini. Aidha, Mhe. Balozi alishauri pia huduma hizo ziweze kupelekwa pia katika Visiwani vya Anjouan na Moheli kwani huko pia kuna mahitaji ya huduma za Afya.