Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro umeandaa maonesho ya biashara ya bidhaa na huduma za Tanzania nchini Comoro tarehe 12 - 19 Desemba, 2022. Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 14 Desemba, 2022 na kufuatiliwa na Kongamano la biashara tarehe 15 Desemba, 2022. Mgeni rasmi wa matukio hayo aliuwa ni Mheshimiwa Kanali Ahmed Abass Ahmed, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. 

Maonesho hayo yalihudhuriwa na taasisi mbali mbali za umma na binafsi, pamoja na wajasiriamali kutoka Tanzania na Comoro. Miongoni mwa waliohudhuria ni pamoja na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT), shirika la Bandari kanda ya Mtwara, Mamlaka ya Mapato Tanzania kanda ya Mtwara, Hospitali ya HiTech, Kampuni za huduma za ARAFAT MULTISERVICE na VERTEX, Benki ya EXIM, pamoja na wajasiriamali wanaojishughulisha na biashara ya bidhaa za chakula, mapambo, na mavazi.