Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Muungano wa Visiwa vya Comoro zimesaini Hati ya Kuanzisha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano. Makubaliano hayo yamesainiwa na Mheshimiwa Dkt. Stergomena L. Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharikia (kwa upande wa Tanzania) na Mheshimiwa Dhoihir Dhoulkamal, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, anayehusika na masuala ya Diaspora na Nchi zinazozungumza Kifaransa (kwa upande wa Comoro) tarehe 14 Februari, 2023 jijini Adiss Ababa nchini Ethiopia. 

Makubaliano hayo ni utekelezaji wa mikakati ya kuimarisha ushirikiano baina ya Nchi mbili hizi kufuatia kusainiwa kwa Hati ya kuanzisha ushirikiano mwaka 2009. Hati hiyo itatoa nafasi zaidi katika kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kiuchumi na kijamii.