TANGAZO: SHINDANO LA UANDISHI WA INSHA

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro kwa kushirikiana na Jumuiya ya Urafiki baina ya Tanzania na Comoro na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Comoro inawatangazia wananchi na wakaazi wote wa Comoro kuwa imeandaa shindano la Uandishi wa Insha kwa lugha ya Kiswahili: 

MADA

  1. Muungano wa Tanzania
  2. Umuhimu wa Kiswahili

Washiriki wanasisitizwa kutumia Kiswahili fasaha na sanifu. Insha hizo ziandikwe kwa mkono. 

Insha zifungwe katika bahasha na kuwasilishwa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Oasis Moroni. Kwa washiriki walioko Moheli na Anjouan wanashauriwa kuwasilisha bahasha zao katika Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wakulima na Wenye viwanda. 

Mwisho wa kuwasilisha INSHA ni tarehe 30 Juni 2022 muda wa saa za kazi.  

Matokeo ya washindi watatangazwa siku ya tarehe 7 Julai 2022 wakati wa Kongamano la Kiswahili litakalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano nambari 2, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro. 

Nyote mnakaribishwa. 

 

 

TAANRIFA

Woubalozi wa Tanzanie ngaoumdjoulizaoni wanaziyoni nane  maranyia wontsi wa Comores na wadjeni ouhossou wourenga founvou harmoi  machindou ya ouandzichi  yaani redaction ( dissrtation):

ZE MADA  ZATSAOULOI:

1.Woumtsangagniho wa Tanganyika na Zanzibari ( Mzalihaniho wa Tanzanie)

2.Manoufaan (Ye faida) yahe lougha ya Kiswahili

 

Ye Redaction yibidi yandzihoi hamhono. Baanda yapvo  naziwasilichoi  harmoi le djoumba la Ubalozi wa Tanzanie  Moroni Oasis.

Ousikou wa mouisso waouwasilicha ze redaction nde tarehi 28 ya Juin 2022.

Namkaribu.