Chini ya usimamizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Serikali ya Komoro kupitia Wizara yake ya Kilimo, Mifugo na Mazingira iliandaa Hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji katika Kisiwa cha Anjouan tarehe 04 Oktoba, 2019. Hafla hiyo ilifanyika katika kijiji cha Vouani, Kusini mwa Kisiwa cha Anjouan kilomita 40 kutoka Mji Mkuu wa Mutsamudu.

Mradi huo ambao unatarajiwa kuanza mapema mwaka 2020 utawezesha nyumba zaidi ya 60,000 kati ya 105,000 kufikiwa na maji. Mpaka kukamilika mradi huo zaidi ya 60% wa wakaazi wa Komoro wanatarajiwa kupata huduma ya maji.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo alikuwa Mhe. Col. Azali Assoumani, Rais wa Komoro. Aidha, Ubalozi uliwakilishwa na Ndg. Mudrick R. Soragha, Kaimu Balozi. Mradi huo unatarijiwa kugharimu zaidi ta USD 50 Milioni mpaka kukamilika.