Kama sehemu ya muendelezo wa ushirkiano katika Sekta ya Afya baina ya Tanzania na Comoro, Hospitali ya Benjamin Mkapa iliopo Dodoma imedhamiria kushirikiana na wadau wa Afya wa Comoro katika utoaji wa huduma za Afya zilizo bora na kwa bei nafuu.

Azma ya utekelezaji wa makubaliano hayo imedhihirishwa kupitia ziara ya Dr. Remigious Rugakingira, Daktari Bingwa wa Urologia kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa, Daktari huyo alifanya ziara ya siku nne Visiwani Comoro ambapo alikutana na wadau kutoka Wizara ya Afya pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje Comoro tarehe 06 Februari, 2019.

Dr. Rugakingira alieleza huduma mbalimbali zinazotolewa na hospitali hiyo, aina ya vifaa vinvyo tumika, wataalamu pamoja na kutoa mapendekezo ya kufanyika (Outreach Program) ambayo itaruhusu kubadilishana madaktari na wanafunzi kwa pande zote mbili.

Kwa mujibu wa Dr. Rugakingira alionyesha kuwa Hospitali hiyo ipo tayari kushirikiana na Wizara ya Afya ya Comoro na kupokea wangonjwa wa Kikomoro ambao wanakuja kufuata huduma za Afya nchini Tanzania. Alichukua fursa hiyo kuwa hakikishia wadau hao ubora wa huduma pamoja na bei nafuu ya huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo.