TAREHE 15 Oktoba 2019 Mufti wa Zanzibar Sheikh Omar Kabbi Saleh Leo tarehe 15 Oktoba 2019 amewasili Visiwani Komoro kwa ajili ya kufanya ziara ya siku tano Visiwani hapa. Ziara hiyo inakuja kufuatia mwaliko aliopewa Mufti huyo na Mufti wa Komoro Sheikh Said Mohamed Toijir..
Katika ziara hiyo Mhe Mufti Kabbi ameongozana na ujumbe wa Watu wawili akiwemo Katibu wa Mufti Sheikh Mohamed Saleh Othman.. Wakati akiwasili Visiwani Komoro, Mhe Mufti na ujumbe wake walipokelewa na Balozi wa Tanzania Visiwani Komoro Mhe Sylvester Mabumba..
Hii ni ziara ya Pili kwa Mufti huyo kufanya Visiwani hapa ambapo mara ya mwisho kufanyika ziara hiyo Ilikua ni Mwana 2015.. Akihojiwa na vyombo vya Habari Visiwani Mufti huyo alieleza kuwa dhumuni la ziara yake ni kudumisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Komoro hususan kwa upande wa Zanzibar ambapo Visiwa hivyo vimekua na ushirikiano wa karibu hasa katika masuala ya Elimu ya Dini, utamaduni, sanaa nk Aidha akiwa Visiwani hapa Mhe Mufti Kabbi na ujumbe wake wanatarajiwa kufanya ziara katika Kisiwa Jirani cha Anjouan pamoja na kushiriki katika Hauli ya Al Habib Omar aka Mwinyibaraka Kama sehemu ya kumuenzi mwanazuoni huyu mashuhuru aliyekulia Zanzibar na kufariki na kuzikwa Visiwani Komoro.





