Mheshimiwa Saidi Yakubu, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro amempokea na kufanya mazungumzo na Bi. Nichola Sabelo, Kaimu Mkuu wa Kituo, Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Comoro aliyefika Ofisi kwake kwa lengo la kujitambulisha. Wawili hao waligusia historia ya ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Ilibainishwa kuwa nchi mbili hizo zinayo historia ya muda mrefu ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali. Kadhalika, nchi hizo zinashirikiana vyema katika Jumuiya za Kikanda ikiwemo Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.