Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Comoro Mhe. Azali Assoumani tarehe 26 Mei, 2019.
Sherehe hizo zilifanyika katika Mji wa Moroni, Visiwani Comoro na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali duniani. Mhe. Makamo wa Rais aliongozana katika ujumbe wake na Mhe. Mwita Waitara, Naibu Waziri TAMISEMI. Wakati akiwa katika sherehe hizo. Mhe. Makamu Rais alipata fursa ya kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Azali Assoumani katika mazungumzo hayo Mhe. Makamu wa Rais alimpongeza Rais huyo kwa ushindi alioupata kufuatia kukamilika kwa zoezi la Uchaguzi hapo tarehe 23 Machi, 2019.
Aidha, Mhe. Makamu wa Rais alimuahidi Mhe. Rais Azali kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Comoro katika nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya Uchumi, Kijamii na ushirikiano katika masuala ya Mila. Sambamba na hilo Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alitoa pole kwa Mhe. Rais Azali kwa maafa yaliyo sababishwa na kimbunga Kenneth kilichopita Visiwa vya Comoro tarehe 24 - 25 Aprili, 2019.
Naye kwa upande wake Mhe. Rais Azali Assoumani alichukua fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono Serikali ya Comoro katika juhudi zake za kuleta maendeleo Visiwani hapa.



