Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro umeadhimisha Sherehe za Miaka 59 ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 2023. Maadhimisho hayo yamefanyika katika kijiji cha Milembeni mkoa wa Itsandaa. Mheshimiwa Siti Farouata Mhoudine, Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja alikuwa Mgeni rasmi. Sherehe hizo zilitanguliwa na zoezi la usafi wa mazingira katika shule ya Msingi Milembeni. Pamoja na mambo mengine, ratiba ya sherehe ilihusisha michezo mbalimbali iliyoshirikisha Wakomoro pamoja na Watanzania wanaoishi nchini Comoro.