Lengo la ziara hiyo ni kuja kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji Visiwani Komoro pamoja na kutanua wigo wa mtandao wa biashara baina ya wajasiriamali kutoka Tanzania na wale wa Komoro. Ujumbe huo pia unatarajia kushiriki kikamilifu katika maonyesho ya biashara yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Komoro kwa kushiirikiana na Mamalaka ya Uwekezaji Visiwani Komoro (ANPI). 

Maonyesho hayo ya biashara yajulikanayo kama Swahili Soko Week Exhibition yanatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Foye de Femme hapa Jijini Moroni ambapo Mgeni Rasmi katika maonyesho hayo atakuwa ni Bi. Saandia Hassani Mke wa Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja. 

Pamoja na mambo mengine, wajasiriamali hao wanatarajia kusaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano na baadhi ya taasisi za Serikali ya Komoro na zile za Sekta Binfafsi. Hii ikiiwa ni sehemu ya  mkakati wa kuendelea kupanua wigo wa ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Komoro. Wajasirimali hao wanatarajia kusaini mikataba ya ushirikiano (MoU) na moja ya maduka makubwa ya bidha za chakula (Super Market) ijulikanayo kama (Sawa Prix) aidha kukundi hicho kitasaini pia mkataba wa ushirikiano na Taasisi  ya Maendeleo ya Wanawake wa Kisiwa cha Ngazidja (CODCOM). 

Hii ni ziara ya pili ya kikundi cha Wajasiriamali wanawake kutoka Tanzania kufanya Visiwani Komoro ambapo ziara ya kwanza ilifanyika mapema mwezi Juni, 2016. Katika ziara hiyo kikundi hicho kiliweza kukutana na kufanya mazungumzo na wanadiapora wa Komoro na kujenga mahusiano ya kibiashara na Diapsora. Aidha wajasiriamali hao waliweza pia kuingia mkataba wa ushirikiano (MoU) ni kikundi cha wajasirimali wanawake kutoka Komoro (EFICOM).