Kikundi cha Afisa mmoja na Askari 14 kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania walishiriki gwaride la kuadhimisha miaka 47 ya Uhuru wa Visiwa vya Comoro tarehe 6 Julai 2022. Kikunid hicho kimeshiriki gwaride hilo kufuatia mwaliko kutoka Jeshi la Visiwa hivyo. Kitendo hicho ni matokeo ya uhusiano mzuri uliopo kati ya majeshi ya nchi mbili hizi na Serikali kwa ujumla. Hii ni mara ya pili kushiriki kwa gwaride la aina hii kwa miaka ya hivi karibuni.