Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umefanikisha ziara ya Mheshimiwa Anissi Chamsidine, Gavana wa Kisiwa cha Anjouan kutembelea Mkoa wa Mtwara Tanzania kuanzia tarehe 02 - 05 Julai 2022. Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano baina ya kisiwa cha Anjouani na Mkoa wa Mtwara. Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Gavana Anissi Chamsidine ameambata na Ujumbe wa Wafanyabiashara 23 pamoja na Viongozi kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye viwanda na Wakulima - Anjouani.