Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeadhimisha siku ya Kiswahili Duniani. Tukio hilo limefanyika tarehe 7 Julai 2022 katika Ukumbi wa wanawake Moroni na kushirikisha Viongozi na wananchi mbali mbali. Mgeni rasmi alikuwa ni Mheshimiwa Djaffar Salim Alloui, Waziri wa Ajira, Kazi, Vijana, Michezo, Utamaduni na Sanaa wa Muungano wa Visiwa vya Comoro. Ratiba ya tukio hilo ilihusisha Kongamano la Kiswahili; na Shindano la Usomaji Makala. Sambamba na matukio hayo, Ubalozi uliratibu Shindano la Uandishi wa Insha ambapo wanafunzi na wananchi kwa ujumla walipata nafasi kushiriki. Tathmini imeonesha kuwa vijana wapatao 50 walishiriki katika zoezi la Uandishi wa Insha na Usomaji Makala.