Mhe. Saidi Yakubu, Balozi mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Comoro amewasilisha leo Jumanne tarehe 28 Mei 2024 Nakala ya Hati za Utambulisho kwa Waziri wa mambo ya Nje Mheshimiwa Doihir Dhoulkamal. Katika mazungumzo yao mafupi Mhe. Balozi alionesha kuwa tayari kufanya kazi kwa ajili ya kuimarisha zaidi ushirikiano uliopo kati ya Tanzania  na Comoro kwa  manufaa ya Watanzania na Wakomoro hasa katika nyanja ya Biashara, Afya, Elimu, na Utamaduni. Ili kufanikisha dhamira hiyo alipendekeza kufanyika mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano tarehe 11-12 Julai, 2-24 ikiwa ni njia moja wapo ya kurasmisha mikataba iliopo kati ya nchi hizi mbili.

 
Kwa upande wake, Mhe. Waziri ameahidi kumpatia ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake mapya na kumtakia kila la kheri .

Mhe,. Saidi Yakubu ni Balozi wa Nne tangu Tanzania kufunguwa Ofisi ya Uwakilishi nchini Comoro