Mhe. Pereira A. Silima, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro ameshiriki uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Precision katika hafla ya iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip Comoro siku ya tarehe 20 Agosti, 2022. Taarifa zaidi zinaonesha kuwa Shirika la Ndege la Precision nimerudisha safari zake nchini Comoro. Shirika hilo litakuwa na ratiba ya safari mara mbili kwa wiki ambapo litakuwa na safari ya kuanzia uwanja wa Ndege wa Anjouan hadi Dar es Salaam kupitia Ngazidja.