Mheshimiwa Pereira A. Silima, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Anissi Chamsidine, Gavana wa Kisiwa cha Anjouani tarehe 12 Januari, 2023 katika Ofisi ya Mheshimiwa Gavana. Wakati wa mazungumzo hayo, Viongozi hao waligusia mikakati ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kiuchumi na kijamii ikiwemo kuhamasisha ufundishaji wa somo la lugha ya Kiswahili pamoja na kuimarisha uzalishaji wa mazao muhimu katika kisiwa hicho.