Mheshimiwa Pereira A. Silima, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro (kushoto) akutana na Sheikh Aboubacar Abdallah Jamal al-Lail, Mufti Mkuu wa Comoro kwa ajili ya kujitambulisha. Viongozi hao wamezungumzia namna ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kijamii. 

Kadhalika, Viongozi hao wamekubaliana kuendeleza mawasiliano ili kuhakikisha wanatekeleza maeneo yatakayoimarisha ushirikiano kati ya Ofisi zao.